Michael Jackson's
Last Performance
Video hii ilichukuliwa kwenye ukumbi wa Staples
Center jijini Los Angeles juni 23
(siku mbili kabla hajafariki) wakati
Michael Jackson akifanya mazoezi kujiandaa na
shoo zake za jijini London,
"This is It"
zilizokuwa zianze mwezi huu.
Video hii inamuonyesha jinsi Michael Jackson
alivyokuwa akiimba na kudansi
wimbo wake maarufu
"They Don't Care About Us"
akionekana mwenye nguvu tele na akilitawala
jukwaa kama kawaida yake.
Video hii itawafanya watu waliokuwa wakidai
kwamba Michael Jackson hana uwezo wa
kufanya shoo kwa ufanisi kama enzi zake
wayameze madai yao.
Wakati huo huo wapenzi wa Michael Jackson
wataweza kuuaga mwili wake kwenye ukumbi
huo huo aliokuwa akifanyia mazoezi
siku ya Jumanne tarehe 7.7.2009.
No comments:
Post a Comment