Monday, July 13, 2009

Waokolewa baada ya

siku 25 ndani ya mgodi

ulioporomoka!



Wang Kuangwei, akitibiwa. Ni mmoja wa watu 3 waliokolewa toka ndani ya
mgodi wa makaa ya mawe uliopromoka. Picha na AP.


Wachina watatu wameokolewa baada ya siku 25 ndani ya mgodi wa makaa ya mawe ilioporomoka Xinqiao, kwenye jimbo la Guizhou, kusini magharibi ya Uchina. Kutokana na taarifa za shirika la habari la China, Xinhua, watu hao wamesalimika kwa kula, udongo na maji machafu ndani ya huo mgodi. Usalama kwenye migodi nchini China ni hafifu sana, na namba ya waliokufa kutokana na ajali za migodi nchini humo ni watu 3200 kwa taarifa za serikali. Inasadikiwa namba ni kubwa zaidi ya hiyo iliyotolewa na serikali ya China.


No comments: