Thursday, July 02, 2009

Wezi wa pin code

wanajaribu kuhonga

wakaa kaunta madukani…



angalia hii ya ATM Skimming



Imegundulika kuwa wezi wa nywila (pin code) za kadi za benki, wanajaribu kuwahonga wakaa kwenye kaunta madukani ili wasome nywila za wateja na wawauzie. Pia wezi hao wanajaribu kuwahonga ili waweke vidude vya kuskimu (ATM Skimming) na kuiba nywila kwenye kaunta. Hayo yameelezwa na kitengo cha upelelezi, makuu ya polisi Oslo. Wateja wanashauriwa kuwa waangalifu wanapokuwa madukani. Wanashauriwa kuwa makini wanapogonga nywila kwenye kaunta, kuwa wajaribu kuzificha hata wakaa kaunta wasizione au ikiwezekana waende madukani na hela taslimu.


1 comment:

Anonymous said...

Sasa jamani tufanyeje? Teknolojia ndo´ipo na inatumika. Wajanja wanatuibia kila siku. Turudi tulikotoka?