Thursday, July 02, 2009

“Biashara haiogombi”

Machangudoa warudi

tena Oslo.




Ma´CD wa Kinaijeria wakiwa mtaani Karl Johans, Oslo.
Picha na Carl Martin Nordby.


Machi Mosi mwaka huu sheria mpya ya kuwabana wateja wa machangudoa nchini Norway ilianza kutumika. Baada ya hapo, ma´CD walipungua karibu kufikia sifuri. Moja ya kipengele cha sheria hiyo ni kuwa mteja akikamatwa na polisi, anatozwa faini. Mpaka sasa wanaume 45 wameshapigwa faini toka sheria hiyo kuanza kutumika.

Toka msimu wa Kiangazi kuanza, machangudoa wamerudi kwa wingi mitaani mjini Oslo. Wengi wa machangudoa wanatoka nchi za Ulaya Mashariki na Naijeria. Kuamkia jana, Pro Sentret, asasi isiyo ya kiserikali ya kuwasaidia machangudoa, ilihesabu wasichana 121 kuanzia saa 23.00 hadi 02.30 Central European Time (CET), kwenye mtaa mkuu hapa Oslo wa Karl Johan. Kati ya hao ma CD, 80 ni wa Kinaijeria. Mkuu wa kituo cha polisi kati Oslo, inspekta Bjørn Åge Hansen ameshangazwa na wingi wa ma CD waliorudi na kuzagaa mitaani. Hii inaonyesha biashara ya kale kuliko zote hapa duniani, bado itaendelea kudumu hata binadamu wakitafuta mbinu za namna gani za kuimaliza, alisema mteja mmoja aliyeulizwa kutoa maoni yake.

No comments: