Wednesday, July 08, 2009

Wizara ya fedha ya Marekani

yashambuliwa na virusi vya

Kompyuta




Toka Julai 4, wizara ya fedha ya Marekani, Kamisheni ya usafari na wizara ya usafiri, zimekuwa zikishambuliwa na virusi vya kompyuta na kusababisha baaadhi ya shughuli zao kukwama. Idara ya Usalama ya Marekani, The US Secret Service ambayo iko chini ya wizara ya fedha, nayo pia imekumbwa na mashambulizi hayo ya TEKNOHAMA.

Tovuti zao zilikuwa zikifanya kazi nusu nusu, baada ya kushambuliwa na virusi. Wizara hizo pamoja na Secret Service wamekataa kutoa maelezo ya mashambulizi hayo, hata hivyo Amy Kudwa, msemaji wa Wizara ya ulinzi wa ndani (Homeland Security Department), amesema kuwa timu ya usalama na madhara ya kompyuta ya wizara hiyo imetoa onyo kwa wizara, idara na vitengo vya serikali kuwa na tahadhari.

Mbali ya Marekani kukumbwa na mashambulizi hayo, Korea ya Kusini nayo imeshambuliwa na vita ya virusi vya kompyuta. Wizara ya ulinzi ya Korea, Bunge la Korea ya Kusini, Korea Exchange Bank, vimepata kipigo cha virusi vya kompyuta, yalisemwa na Ahn Jeong-euan, msemaji wa shirika la usalama wa habari la Korea ya Kusini.


No comments: