Atuma hela Panama
zimechukuliwa Mexico!
Dada mmoja Mpanama alituma hela kwa mtandao wa Estern Union kwa mama yake anayeishi Panama City kama kroner 2000,- (Dala za Kimarekani 327,- au T.shs. 443 541,- kwa bei ya leo) Julai 20. Lakini hela hazikufika Panama, badala yake zilifika Mexico na zilichukuliwa mara moja. Nini kimetokea au nani amezichukua hizo hela haielewiki, huyo dada ameliambia gazeti la kila siku hapa Norway la Aftenposten. Dada huyo amesema kwa miaka sita sasa, amekuwa akituma hela kwa mama yake mzazi kwa kutumia ofisi za Western Union. Hivi karibuni alianza kutumia mtandao kutuma hela kwa mama yake.
No comments:
Post a Comment