Sikiliza dada huyu
yale yale ya nywila
(koda/password)
Huyu dada ameolewa na ana watoto wawili,yeye anajishughulisha na biashara ya kuuza nguo za kike,mumewe ni mfanyakazi ofisini katika kampuni fulani hapa Dar huyu dada analalamika kuwa mumewe amekuwa na kawaida akirudi tu nyumbani anazima simu zake au kuzificha na akiziweka juu basi zina password mpaka kwenye phonebook,sms,yaani kila folder katika simu ina password ...sasa wiki iliyopita akamuuliza mumewe kwa nini huwa anaficha/kuzima simu na zina password? mume akamwambia anazima maana watu wa ofisini wanakuwaga wanamsumbua,mke haikumuingia akilini..haya kwa nini unaweka password?ooh watu ofisini wana tabia mbaya wanakawaida ya kupekua simu za watu na kujipunguzia salio wakati mwingine.Mke akamwambia sawa ila naomba simu uwe unaziweka pale kwenye meza ambapo hata mimi naweka simu yangu mume akasema poa.
No comments:
Post a Comment