Jaji Frederick Mwita Werema
ateuliwa kuwa
Mwanasheria Mkuu wa serikali
Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Jaji Frederick Mwita Werema kuwa mwanasheria mkuu mpya kuchukua nafasi ya Jaji Johnson Mwanyika ambaye anastaafu.
Mheshimiwa Rais amemteua pia Bwana George Mcheche Masaju kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu, uteuzi huo unaanza mara moja. Kabla ya kuteuliwa kuwa mwanasheria mkuu, Bwana Werema alikuwa Jaji katika mahakama kuu kitengo cha Biashara, wakati Bwana Masaju alikuwa ni mshauri wa mambo ya kisheria wa Ikulu.
No comments:
Post a Comment