Mabadiliko makubwa
ya intaneti kufanyika toka
ianzishwe miaka 40 iliyopita
Hivi karibuni kutafanyika mabadiliko makubwa ya intaneti, toka ianze kutumika miaka 40 iliyopita. Hayo yamesemwa na shirika la kuthibiti intaneti – ICANN (Internet Corporation for Assigned Names and Numbers.
ICANN inasema iko katika mpango wa kubadili anwani za mtandao zitakazokuwa na herufi za lugha zingine badala ya kutumia herufi za Kilatini pekee. Hadi sasa herufi zinazokubalika kutengeza majina ya anwani za mitandao ni 26 tu za Kilatini.
Kama mabadiliko hayo yakikubaliwa kwenye mkutano mkuu utakaoanza Oktoba 30, maombi ya kwanza yatakubaliwa kuanzia Novemba 16 mwaka huu. Na ICANN inatarajia kuwa kuanzia katikati ya 2010, anwani za intaneti zenye herufi za lugha zingine zinazoishia kivingine; zitaanza kutumika.
Kwenye ufunguzi wa kikao cha kamati ya utendaji ya ICANN mjini Seoul, Korea ya Kusini; Rod Becktrom wa ICANN anasema sababu zilizofikia kufanya mabadiliko hayo ni kuwa nusu ya watumiaji wa intaneti (ambao wanafikia watu bilioni moja na nusu duniani kote) wanatumia lugha zenye herufi zaidi ya 26 za Kilatini.
Kwenye kikao hiki kinachoendelea mjini Seoul watazungumzia jinsi ya kutumia jina mama (domain) kama ”dot com”, ”dot net”, ”dot org” n.k.
Kama wakifikia makubaliano kwenye kikao hiki, basi kuna uwezekano wa kuwa huru kwa watumiaji wa intaneti, kutengeneza anwani za intaneti zitakazokuwa zinaishia na majina mama wanayotaka, kitu ambacho hadi sasa hakikuwezekana.
Mtu anaweza kujitengenezea tovuti inayoishia kama atakavyo, kama mfano unavyoonyesha hapo chini:
http://www.chamachawatanzania.oslo.norway
http://www.ubayaubwela.maneromango
Imeandikwa na mhariri wa blogu
No comments:
Post a Comment