Tuesday, October 27, 2009

Marubani wasahau kutua:

Sababu: walikuwa busy na

Kompyuta paja (lap top)



Wiki iliyopita, ndege ya shirika la ndege Northwest Airlines, Airbus A320 ikiwa na abiria 144 ikitokea San Diego kuelekea Minnesota, ilipotea kwenye rada ya uwanja wa St. Paul International mjini Minneapolis, kabla ya kutua. Sababu marubani walijisahau kwenye kompyuta paja. Ndege hiyo ilipita kwenye huo uwanja, ikaendelea dakika 16 kabla ya marubani hao kushtuka na kurudi na kutua kwenye uwanja huo.

Marubani hao wamesimamishwa kazi.

No comments: