Saturday, October 24, 2009

Majira ya theluji




Saa 9 usiku kuamkia Jumapili, 25 Oktoba 2009, hapa Norway (Skandinavia) tunabadili majira na kuingia majira ya theluji (Winter time). Kufuatia na mabadiliko ya majira, tunarudisha saa nyuma. Sasa hivi tuna tofauti ya masaa mawili na saa za Afrika Mashariki.

Mfano:

Hapa Norway ikiwa saa 4 za asubuhi,

Tanzania (Afrika Mashariki) ni saa 6 za mchana...

Mabadiliko ya saa hufanyika mara mbili kwa mwaka.

Jumapili ya mwisho ya Machi, kuingia majira ya Kiangazi (Summer). Tunasogeza saa moja mbele. Tofauti ya saa moja na Afrika Mashariki.

Jumapili ya mwisho ya Oktoba, kuingia majira ya theluji (Winter). Tunarudisha saa moja nyuma. Tofauti ya masaa mawili na Afrika Mashariki.

No comments: