Thursday, October 08, 2009

Mohamed Raza:

Mafisadi wanafanya nini

Kamati Kuu?



MFANYABIASHARA maarufu wa Zanzibar na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM, Mohamed Raza amesema ni vyema wale wanaotuhumiwa na ufisadi waliomo katika Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC) wakajiengua.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Star Light mjini Dar es Salaam, Raza alisema cha kushangaza zaidi ni kwamba miongoni mwa wanaotuhumiwa wako kwenye kamati ya maadili ya chama hicho.

Alisema watu hao wanaotuhumiwa kwa ufisadi walioko kwenye Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na bungeni, wangejiondoa ili kulinda heshima zao na chama chao.

Mohamed Raza

Mohamed Raza

“Mtu mzima akipewa tuhuma yakhe, hukaa pembeni, huo ndiyo ustaarabu,” alisema Raza ambaye hakuwa tayari kutaja majina yao lakini akasisitiza kwamba wanajulikana.

Alisema kujiondoa kwa watuhumiwa hao kutamsaidia Rais Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho aliyeko msitari wa mbele katika kupiga vita ufisadi.

Raza alimsifu Spika wa Bunge, Samwel Sitta kwa msimamo wake uliolifanya Bunge kuwa la aina yake katika kusimamia maslahi ya wananchi, hasa katika vita dhidi ya ufisadi.

‘Kama siyo Bunge, Tanzania leo tungekuwa watumwa. Tanzania ingekuwa ya matajiri wachache,” alisema....bofya na endelea>>>>

No comments: