Wednesday, October 07, 2009

Tuungane na wanaotutafuna?



Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo

Mpenzi wa enzi,

Usiogope. Sikutungii tenzi lingine bovubovu au tuseme tenzi nalitunga kila siku ila linakaa moyoni mwangu usije ukadhani kwamba ubovu wa vina vyangu ni ubovu wa mapenzi yangu kwako. Mapenzi yashamiri hata kama nakosa maneno ya kuyaelezea.

Vipi hali yako wiki hii? Nakuwazia hadi kichwa kinawanga. Natamani kusikia sauti yako inayonguruma na kumwaga radi na kuona ndevu zako zikichezacheza wakati unacheka kidogo. Nikiwazia hivyo natabasamu mwenyewe huku nikingojea kwa hamu kuwa na wewe tena.

.....bofya na endelea>>>>>

No comments: