
MTOTO Mwinyi Said (6) aliyekuwa anaishi na wazazi wake Gongolamboto jijini Dar es Salaam, hivi karibuni ameuawa kikatili kwa kuchomwa kisu kichwani, kutolewa ubongo, kukatwa koromeo kisha mwili wake kutupwa kwenye karo la choo.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Septemba 13, mwaka huu ambapo inaelezwa kuwa wakati mtoto huyo anafanyiwa unyama huo alikuwa ametumwa dukani kununua bidhaa mbalimbali.
Akiongea na Uwazi juzi, baba wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Said Hussein alisema kuwa, siku hiyo Mwinyi alikuwa ametumwa na dada yake kwenda kununua majani ya chai na kibiriti lakini cha kushangaza giza liliingia bila mtoto huyo kurudi nyumbani.
“Tulichukua jukumu la kuanza kumtafuta kila kona lakini hatukufanikiwa kumpata, ndipo tuliporejea nyumbani ili kuweka mikakati mingine ya kumpata na tukakubaliana kwenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Gongolamboto,” alisema Said.
Akaongeza kuwa, baada ya kuliripoti tukio hilo polisi, Septemba 17, mwaka huu mchana walifika watu wa zima moto katika moja ya karo lililokuwa jirani na nyumba yao na kuanza kulibomoa kwa maelezo kuwa, kulikuwa na harufu mbaya iliyokuwa inatoka humo..
No comments:
Post a Comment