Wednesday, October 07, 2009

Vijana wa kazi kushirikiana na UDI





Septemba 25, idara ya usalama wa taifa ya Norway; Politiets sikkerhetstjeneste (PST) na idara ya uhamiaji ya Norway; Utlendingsdirektoratet (UDI) zimetiliana saini mkataba wa kushirikiana. Kuanzia sasa idara hizo mbili zitakuwa zinashirikiana kupeana habari za waombaji wa kuishi hapa Norway. UDI wanapaswa kuwaambia PST lolote wanalojua kama wanamtilia mtu mashaka, ili PST wafanye uchunguzi wa kina wa mwombaji. Nao watoto wa kazi; PST wakiwa na jambo la mtu, watapaswa kuwatonya UDI. Kabla ya makubaliano hayo; idara hizi mbili hazikuwa na uhusiano unaojulikana rasmi.


No comments: