Friday, November 13, 2009

Duh!

Binti wa Kiislamu na ulimbwende



Hamida Hassan na Imelda Mtema

Baraza Kuu la Waislamu nchini, BAKWATA limesema si haki wala halali kwa mabinti wa kiislamu kushiriki mashindano ya urembo kwa vile yanadhalilisha wanawake kwa kuwaweka nusu nguo, nusu utupu, Ijumaa linashuka sanjari na mtoa tamko hilo

Akilipa elimu gazeti hili, Naibu Katibu Mkuu (Dini) wa BAKWATA, Mohammed Hamis Said alisema kuwa, hii ni mara ya pili kwa chombo hicho cha juu cha mshikamano wa kiislamu nchini kutoa tamko kuhusu mashindano hayo.

“Suala hili tulishaliongelea sana na kutoa tamko kuwa, ni haramu kwa mwanamke wa kiislamu kushiriki mashindano hayo lakini kwa sababu nchi inaenda na utandawazi na maendeleo hakukuwa na jinsi,” alisema Said.

Aidha, Naibu huyo alisema kuwa, uozo uliopo sasa nchini ni kitendo cha baadhi ya watu kufuata tamaduni za nje (Magharibi) na iwapo wao (BAKWATA) wataingilia swala hilo kwa undani zaidi watakutana na sheria inayowabana kutoka kwa jamaa wa haki za binadamu, “hivyo swala hili linabaki kwa mtu mwenye jina la kiislamu na si mwislamu,” alisema.

Alifafanua zaidi kwamba, anavyojua yeye, mabinti waislam wanaoshiriki mashindano ya u-Miss wana majina ya kiislamu lakini si waislamu kwani mtu anayefuata maadili ya kiislamu kamwe hawezi kushiriki mashindano hayo.

Nao baadhi ya waumini wa imani hiyo, walisema kuwa, wamechoshwa na mashindano hayo na kuwalaani wazazi wanaowaruhusu binti zao kwenda kushiriki mashindano hayo kuwa, hawajui wanachokifanya kwani wanamruhusu mtoto kukulia katika maadili ya kishetani.

“Unajua kumwacha mtoto wako akaingia katika mashindano ya urembo ni kumdhalilisha yeye na wewe mzazi, kwanza kwa itafika mahali binti wa Kiislamu akishiriki tunamchapa bakora hadharani,” alisema mama Husna akisema yeye ni mkazi wa mtaa wa Songea, Ilala jijini Dar es Salaam.

Toka Global Publishers


5 comments:

Anonymous said...

Hehehee
Basi waweke mashindano ya hijabu
na tutashindana nao vile vile

Jamaldeen T. Bin Mazar E. Shariff Ibn Zenjibari said...

Hawa jamaa sijui wanaishi karne ya ngapi? Waache basi kuangalia luninga, waache kutumia simkono, waache kupanda ndege na magari. Manaake vitu hivi havikuwepo enzi hizo. Kama kila kitu tutakuwa tunaangalia na kusikiliza tu bila kutumia akili zetu kama binadamu, basi hatuwezi kufika mbali.

Mambo mengine waachiwe binadamu wenyewe waamue. Kwanini binadamu wengine wanataka kuamua kwa ajili ya binadamu wengine?

Waachiwe....Mwenyezi Mungu kaumba binadamu watumie akili zao.

Kama ni dhambi wanafanya, basi...watakiona jehanam...Na kama ni dhambi...Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye....

Samahanini kwa watakaosoma hili na kuona kama nimekashifu Uislamu.

Anonymous said...

Jamaldeen,

Simkono ni nini?

Jamaldeen T. Bin Mazar E. Shariff Ibn Zenjibari said...

Simkono nimelitotoa kutoka simu ya mkononi...


Wikiendi njema!

Anonymous said...

Asante mkuu!