Monday, November 23, 2009



A Golden Opportunity? from : posted by KAIROS Canada on Vimeo.


5 comments:

Mkongo said...

Tanzania haki iko wapi? Tutaiendekeza CCM mpaka lini?

Najumuika Ulingoni kuwaonyesha link yenye video ya yaliyotokea mwaka 1996 huko Bulyanhulu wakati wananchi walivyoondelewa kwa nguvu bila huruma na uvunjaji wa haki, tena nchini kwao kumbuka serikali yao walioiweka madarakani ndiyo waliofanya vitendo hivi.

Pia Rais wao Jakaya Mrisho Kikwete amewadanganya wakati wa kampeni... nasema NAMCHUKIA kwasababu ni Mnafiki.

Hata faida inayopatikana na machimbo haya haiwafaidishi wananchi hawa ni kwa viongozi wachache ambao wanapenda kujinunulia magari ya kifahari. kuishi maisha ya kifahari, kujilipa mishahara minono, wenye sifa ya umimi na sio mimi na wewe na yule. Jamani tuwaonee huruma asilimia kubwa ya wananchi vijiji wanaoishi kwa maisha ya tabu.

Asante kwa waliotengeneza video hii kutuonyesha yaliyotokea huko. Mimi binafsi nimesikitika sana na imenigusa.

Asanteni

Anonymous said...

Hii video imenisikitisha sana. Haya ni mazibitisho ya myonge kutokuwa na haki.

Tamaa ya utajiri ya viongozi wetu imekuwa kubwa kiasi kwamba huruma na ubinadamu umewatoka.

Nina uhakika kwamba kuna kesi kama hizi nyingi. Sisi kama watanzania hasa tuliopo nje inabidi tuanza kampeni ya kutetea haki za watanzania wenzetu wasio kuwa na sauti.

Mwanzo unaweza kusambaza hii video katika vyombo mbali mbali vya habari na organizations kama Amnesy International nchi za nje.

Naelewa kwamba nchi zinazotoa misaada kwa mfano Nowray, zinajua kitu gani kinachoendelea. Lakini hata hivyo tusikae kimya labda kuna watu wanaweza kuchukua hatua ya kuwabana viongozi wa nchi kubadilisha tabia kama wanataka uhusiano na nchi zingine.

INABIDI TUSHIRIKIANE KUPIGANIA HAKI ZA WANYONGE. NATUMANI POSITIVE RESPOND.

Anonymous said...

Angalia sasa sijui mkono wa serikali au vipi. Video imeshaondolewa!!!!

Anonymous said...

Hata kama video imeishatolewa, bahati nzuri tumeweza kuisambaza katika vyombo mbali mbali. Hivyo nyie mlio husika kaeni mkao wa kula.

Anonymous said...

Pongezi kwa Tanzania Association Oslo na Vimeo kwa Video ya Mauaji ya Geita Gold Mines,ambayo imeondolewa.Hata hivyo ukweli umeshaonekana,karibuni Duniani kote na wahusika wanaeleweka.Kotokana na Mauaji hayo ambayo yamesikitisha wengi,wahusika ambao ni Watawala wa Awamu ya Tatu[1995-2005]Rais Mkapa,Waziri Shija,Kiwelu nawengineo,kumbukeni kuwa Mwenyezi Mungu ameona Maovu yenu,mtashinda hapa Duniani lakini Mahakama ya Mwenyezi Mungu hamtashinda,na hamtapata Amani hata kidogo,na dalili zimeshaanza kuonekana hapa Duniani.