Polisi aiba kroner milioni moja

Mama mmoja polisi ameshtakiwa kwa kuiba kroner milioni 1.1 kati ya mwaka 2003 na 2007. Mama huyo aliiba hela za gharama za pasipoti na hela za gharama wageni wanazolipa kuombea vibali vya kazi na vya kuishi. Alikuwa anafanya kazi kwenye kituo cha polisi cha Vestoppland. Mama huyo anachunguzwa na kitengo maalumu cha polisi kinachoshughulikia ufisadi ndani ya jeshi la polisi, hayo yamethibitishwa na msemaji wa kitengo hicho, Bi. Liv Marit Sylliåsen.
No comments:
Post a Comment