Waswiss wapiga kura
kukataa misikiti yenye
minara!
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh_5gIoSEm3xtgumdKqbRHP2U5AhEeJoMWW1SuLnxw4UbyWIbd6nqyptVm7cXLZz7pxfT6RChkCChDXy_9ZdhfIuMzbzpHrzEfRQrD_JtKp4Dh8e5Cfy9iNuCKzxzUJg12defdKBqrOvx3E/s320/Mosque+in+Geneva.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhTvIml8B0FrMtTMhpnmoYkBBUccBNf-FlJd5N61yFnD4JHmKgvUihh-5qrRF7hbnPC0X4p4nCJ4kzKOXVAhZuHXhTy7447o7LMXGjIjs0XNSgHOvxu-GYROurrhdLQ9pTLfJ7wl86JwW89/s320/SVP+anti-minaret+poster.jpg)
Bango la kampeni la chama cha SVP.
Jana Jumapili Waswiss wamepiga kura ya maoni na kukataa kwa wingi wa kura zaidi ya asilimia hamsini na saba kujengwa kwa misikiti yenye minara nchini humo. Chama cha wahafidhina wenye siasa kali zenye kupinga wageni nchini humo; Swiss People´s Party (SVP), ndicho kilichosababisha upigaji huo wa kura za maoni. SVP wanasema minara kwenye misikiti ni ishara na dalili za kuenea kwa Uislamu. Wachunguzi wengi wa mambo ya kijamii na kisiasa wanadai kuwa wingi wa kura hizo si za kupinga minara tu kwenye misikiti, bali ni za kupinga mambo yanayofanywa na Waislamu wenye siasa kali za uhafidhina, ambayo yanapingana na demokrasia za nchi za Magharibi. Hizo ni ishara za Waswiss kuhofia Uislamu.
Waziri wa sheria wa Uswiss, Bi. Eveline Widmer-Schlumpf amesema kuwa wanaangalia jinsi gani wingi huo wa kura za maoni utakavyoingizwa kwenye sheria za nchi hiyo.
Kwa sheria za Uswiss, chama chochote kinachoweza kukusanya saini za watu 100 000 tu kinaweza kuitisha kura ya maoni ya nchini nzima. Na hivyo ndivyo SVP ilivyofanya, na kuweza kuitisha kura hiyo ya maoni. Kwa kipindi cha miezi 18, SVP imefanya kampeni ya kuokota hizo saini. Kuna Waislamu 400 000 na misikiti mine tu yenye minara.
Kura hizo za maoni zimeshtua wapenda haki za binadamu duniani, lakini vile vile zimeamsha hamasa kwa vyama vingine vyenye siasa kali za uhafidhina na wasiopenda wageni, kuhimiza kura za maoni za namna hizo kwenye nchi zao. Nchini Ufaransa kumekuwa na kampeni kubwa za kupinga wanawake kuvaa hijabu na mabaibui makazini na mashuleni na walioendesha kampeni wamefanikiwa. Hijabu na mabaibui yamepigwa marufuku makazini na mashuleni. Nchini Ujerumani, kumekuwa na mikingamo ya kupinga kujengwa kwa msikiti mkubwa kuliko yote iliyoko Ulaya Magharibi.
Imeandikwa na mhariri wa blogu.
Bofya na angalia:http://www.islamophobia-watch.com/
Bofya na angalia:http://infidelsunite.typepad.com/
No comments:
Post a Comment