Monday, November 30, 2009

Waziri wa sheria:

Kuziba nyufa za sheria za

wageni kuingia Norway


Waziri wa sheria, Knut Storberget


Waziri wa sheria, Bw. Knut Storberget, amesema leo kuwa ana mpango wa kupeleka mswada Bungeni (Stortinget) wa kuzuia mtiririko wa watu wanaokuja kuomba hifadhi za ukimbizi. Amesema kuwa Norway itashirikiana karibu sana na nchi za EU kuhakikisha kuwa wanaoingia nchini ni kweli wana hadhi ya kuomba ukimbizi.

Storberget ameongeza kuwa inawezekana kabisa kuzuia watu kuingia kiholela bila kuvunja haki za binadamu. Mswada huo utawakilishwa Bungeni mwakani.

No comments: