Sunday, December 27, 2009

Aibu Julius Kambarage Nyerere International Airport



Wadau wa Oslo  habari ya muhimu sana naomba mwiiposti ili watu waelewe kinachoendela hapo uwanja wa Ndege wa Julius Kambarage Nyerere (JKN)


Umekua ukisikia mara kwa mara vituko vya uwanja wa ndege wa JKN kuanzia kuibiwa , kusachiwa kwa baadhi ya abiria , kulaghaiwa na aina nyingine nyiingi sana za uharamu ndani ya uwanja huo kutokana na ukuaji wa teknolojia hata hawa wezi na matapeli nao wanapandisha viwango hata aina nyingine za uharamia wao .


Kwanza ni kwenye sehemu za kupitisha mizigo inayotoka na kuingia nchini sehemu hiyo imejaa watu mbalimbali wanaohusika na usalama wa uwanja na watu wanaotumia uwanja ule watu hawa kushirikiana na madukani ndani ya uwanja huo ya kuuza vitu ambao ni wadau wakubwa wa wizi unaoendelea ndani ya uwanja .


Kama umewahi kuibiwa kitu kama laptop hatua ya kwanza ni kutoa taarifa hapo uwanjani mara nyingi watasema vitu vyako vimeibiwa Nairobi au Kilimanjaro na Ethiopia ukweli ni kwamba vitu hivyo huibiwa na watu wa (majina kapuni kwa sababu maalum za maadili), sehemu za kwanza kuuzwa au kuhifadhiwa ni Duka namba nanihii ambao kuna Huduma za Internet. 


Duka hilo hujaa mali zilizoibwa ndani kwa kujidai Used Vimetoka Ulaya na Bara Asia. Duka hilo hilo kama una haraka na kupanda ndege watakuuzia hata Vocha za simu ambazo zimeshatumika na ukiondoka umeliwa


Saa zingine Abiria anaweza kua amefanya kosa badala ya askari kumchukulia hatua anaweza kulazimishwa kuachia Laptop yake au Kamera ili mradi ni kifaa kinachouzika haraka ndio maana ndani ya maduka hayo vifaa vile havina charge battery na vifaa vingine vya kuviwezesha kufanya kazi kwa uhakika .


Ukizunguka upande wa Pili kuna duka la kuuza vyakula kuna mtanzania mwenye Asili ya ki-Asia ukizungumza nae kwa upole na vizuri anaweza kukuuzia laptop hata kamera ambazo husahauliwa au huibwa katika mgahawa anaousimamia uwanjani hapo kwa jina la (kapuni) .


Ukienda mbele kidogo Kuna duka la ziada Nalo la vitu vidogo vidogo kuna kijana mwenye asili ya visiwani kazi yake kubwa ni kununua simu zilizoibwa uwanjani hapo ni mtaalamu wa kubadilisha hizo simu ziweze kutumika Tanzania .


Ndani ya duka iloilo wauzaji wa Tiketi bandia za kusafiria wapo na ukitaka ni bwerere haswa za mashirika yetu ya ndani kama Air Tanzania , Precision Air na ZanAir .


Ukikaa uwanjani usishangae kuona askari polisi anatoka kwenda kwenye gari ya msafiri mara nyingi ni kwenda kupeana cha Juu.


---Mdau uwanjani JKN---

No comments: