Saturday, December 26, 2009




Ama kweli mnene hawezi kuelewa minyoo ya mwembamba



Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.


Mpenzi wangu Frank,


YAANI nimesikitika!  Nilikuwa nimemwomba Mama Bosi anipe angalau siku mbili nije nikuone mpenzi wangu, tena nikushtue bila hata wewe kujua unipate mimi kama zawadi yako ya Krismasi. 


Tena MB akakubali lakini nilipokuwa najiandaa kwenda kukata tiketi ya basi huku moyo wangu unaimba Frank Fleva ya nguvu kwa raha ya kumwona mpenzi wangu tena, ghafla MB akaniambia kwamba hawezi kuniruhusu eti amegundua Krismasi hii kutakuwa na wageni wengi sana hivyo ananihitaji. 


No comments: