Saturday, December 26, 2009

Theluji ya karne yaanguka mashariki ya Norway


Magari yamefunikwa na theluji


Kuanzia jana jioni kuamkia leo Jumamosi, theluji nyingi ya karne imeanguka mashariki ya Norway. Theluji nyingi ya namna hii haijawahi kuanguka mjini Oslo kwa miaka mingi toka upimani wa kisayansi wa kuanguka kwa theluji ulipoanza karne iliyopita!


Watu wanashauriwa kuacha magari yao na kuchukua usafiri wa umma wakisafiri. Neel Irgens wa mamlaka ya barabara, anasema kuwa mamlaka hiyo inawahisi watu kukaa nyumbani kama hapana ulazima wa kutoka kwenda sehemu yoyote ile. Ajali ndogo ndogo nyingi za kugogangana kwa magari zimeripotiwa hapa Oslo. Hayo yameripotiwa na mkuu wa operesheni wa polisi Oslo, kamanda Finn Belle.

No comments: