Monday, December 21, 2009




Lionel Messi mchezaji bora wa soka 2009, Marta bora kwa soka la wanawake.









Marta (Brazil) na Lionel Messi (Argentina) wachezaji bora wa soka 2009



Kwenye hafla iliyofanyika Zurich leo jioni kwenye makao makuu ya FIFA, Mwajentina na mchezaji wa Barcelona, Lionel Messi amechaguliwa kuwa mchezaji bora mwanamme wa soka kwa mwaka 2009. Messi amewapiku Christiano Ronaldo (Real Madris, Ureno), Andres Iniesta (Barcelona, Hispania), Kaka (Real Madrid, Brazil) na Xavi (Barcelona, Hispania). Kwa upande wa soka la wanawake, Mbrazil Marta amekuwa mchezaji bora kwa soka la wanawake. Hii ni mara ya nne mfululizo kwa Marta kuwa mchezaji bora wa dunia, mara ya kwanza 2006. Ronaldo amepata tuzo ya Ferenc Puskás ya goli la mwaka 2009. Ronaldo alifunga goli hilo, kwenye robo fainali kati ya Manchester United na Porto. Goli alilofunga Ronaldo lilipimwa likiwa kwenye kasi ya kilomita 102 kwa saa, kipa Helton wa Porto hakuona kitu.


FIFA imetangaza wachezaji wa timu bora ya 2009 (FIFA Pro World XI). Ni wachezaji wa Premier League (Uingereza) na La Liga (Hispania)


Golikipa: Ike Casillas (Real Madrid)


Walinzi: Dani Alves (Barcelona), John Terry (Chelsea), Nemanja Vidic (Manchester United), Patrice Evra (Manchester United)


Viungo: Xavi (Barcelona), Andres Iniesta (Barcelona), Steven Gerrard (Liverpool)


Washambulizi: Lionel Messi (Barcelona), Christiano Ronaldo (Real Madrid), Fernando Torres (Liverpool)

No comments: