Tuesday, December 22, 2009

Risala nzuri tu ya marehemu umeme ambayo imekuta ikitandazwa katika simu za mkononi duniani kote.




RISALA FUPI YA MAREHEMU UMEME 





Marehemu alizaliwa 1976 huko Kidatu Tanzania Bara. Katika uhai wake aliwatumikia Wazanzibar kadri ya uwezo wake, marehemu alisumbuliwa na maradhi mbali mbali kama vile kukatika mara kwa mara na mgao.


Wakati wa Salmin aliwahi kaufleti kwa kipindi cha Ramadhani hadi siku kuu na serikali kuamua kuongeza sikukuu ya tano. Mnamo mwaka 2008 aliwahi kufleti kwa muda wa siku 28,na kufanikiwa kurudia hali yake ya kawaida kwa msaada wa madaktari kutoka Norway.


Mnamo tarehe 10.12.2009, marehemu alikuwa katika matibabu na madaktari kutoka Afrika Kusini, lakini hawakufanikiwa na kupoteza maisha Katika kijiji cha Fumba Zanzibar.


Katika uhai wake marehemu alifanya mengi ikiwemo kumulika watu na mali zao pamoja na kukuza uchumi. Marehemu ameacha watoto wawili, GIZA na JOTO. WAKE 2,TABU YA MAJI na HARAMA ZA NAULI KUPANDA, na MAHAWARA 2. Mapacha,DIZELI na PETROLI.


MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI.


AMIN

1 comment:

Jamaldeen T. Bin Mazar E. Shariff Ibn Zenjibari said...

Risala nzuri. Sijui tatizo la umeme Zanzibar litaisha lini....