Napendekeza kuanzishwe MJADALA wa kuzungumzia kuhusu mustakabali wa kujiendeleza kielimu kwa watanzania wanaoishi Norway . Mjadala huo utawahusisha pia magwiji wa elimu watakaotoa mada mbalimbali kuhusu elimu inavyobadilisha maisha ya watu na nini kifanyike jamii yetu inayoishi hapo Norway ifanye ili kuweza kujiendeleza.
Mjadala huo uwahusishe pia ubalozi wa Tanzania pale Sweden ambao watatueleza jinsi serikali yetu itakavyoweza kusaidia kuchangia katika mikakati yetru kujikwamua kielimu hapa Denmark. Mijadala kama hii iwe ya kudumu na ipangwe kufuatana na mikakati tutakayojiwekea. Kwa kuwa Chama Cha Watanzanai wa Norway ndicho chombo kinachowaunganisha watanzania wanaoishi Norway wa ujumla wake, ichukue jukumu la kuandaa mjadala huu wakituhusisha wote katika maandalizi.
Hatma ya maendeleo ya mtanzania anayeishi nje ya nchi yake ni chimbuko la maendeleo kule Bongo kwani katika juhudi zetu tunazofanya kujikwamua kiuchumi tunachangia sana katika uchumi wa Tanzania.
Wote tunaelewa kuwa pamoja na maisha magumu tuliyonayo, lakini pia tunatuma fedha nyumbani kusaidia ndugu na jamaa zetu pamoja na kuendesha miradi mbalimbali ya biashara. Hivyo ni vyema kabisa wakati wa majadiliano haya tukauusisha ubalozi wetu ili kama serikali watueleze watakavyochangia. Tusipotumia fursa zilizoko hususan zinazotolewa na serikali yetu, pesa hizo au fursa hizo zitaenda kwa watu wengine. Tusifikiri eti kama hatutazitumia zitabaki zinatungojea tu mpaka tuzinduke usingizini. Kuna fursa nyingi sana ambazo balozi zetu zinatoa kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi lakini hatuzijui.
Hivyo huu ndio wakati wa kuzijua na kuzitumia. Kwa mfano, kuna scholarships ambazo serikali inazitoa kwa watanzania kusoma na sio lazima wawe pale nyumbani tu hata wanaokaa nje wana nafasi na haki ya kuzipata! Tuufanye mjadala kama huu kuwa ndiyo nguzo imara ya kujiimarisha sisi watanzania wote! Wakati tunaipenda nchi yetu, tujipende kwanza kwa kujiendeleza. Sisi tunaoishi nje ya nchi tunayo nafasi kubwa zaidi ya kufanikiwa kuliko watanzania wanaoishi pele Bongo! Tujadiliane!
No comments:
Post a Comment