Afariki kwa kulipukiwa
na pipi ubani mdomoni
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhTi3QS1iz2QPBj5ItEfE2rOhishLLu1DrxWtAo3LYGSMSFLTOU7evc4yvq0bS7ee56h3AlxoaO1O12oMZ6_bXOcwZldzSVDL_UGT-a6R6z-0eAGDhIDuNrfpIvdmuuYuFWFkJw4VtIR5Ga/s400/i-do-like-my-chewing-gum.jpg)
Vladimir Likhonos (25) amefariki dunia baada ya kulipukiwa na pipi ubani mdomoni. Vladimir alikuwa mwanafunzi wa kemia kwenye taasisi ya kemia ya Chuo Kikuun cha Kiev nchini Ukraina. Aliichovya pipi ubani kwenye poda kemia kabla ya kuanza kuitafuna, ghafla bin vuu, pipi ubani ikalipuka na nusu ya uso wake kupasuka kwa mlipuko.
Mwanafunzi huyo wa kemia alikuwa na tabia ya kuchovya pipi ubani kwenye tindikali limao ili kuongeza utamu. Bahati mbaya, akawa amejisahau na kuichovya kwenye poda kemia kabla ya kutafuna.
1 comment:
Inabidi darasa la kiswahili lifunguliwe.
Pipi ubani ni 'Big G'?
kemia poda ni nini?
Post a Comment