Thursday, December 10, 2009

Obama kutua saa 2.45 asubuhi

Saa za Ulaya ya Kati (CET)



Rais Obama anatarajiwa kutua na Air Force One kwenye uwanja wa ndege Oslo Gardemoen, kama maili 50 nje ya Oslo. Kama hali ya hewa ikiwa nzuri ataletwa mjini Oslo na msafara wa magari. Njia ya kuja Oslo kutokea Gardemoen E 6 itafungwa mpaka msafara wa Obama ufike Oslo. Kama hali ya hewa itakuwa kama ilivyo ya theluji na mvua za manyunyu, basi atarushwa na Marine One (helikopta, moja ya vyombo vya usafiri vitakavyokuja naye) na kutua kwenye kasri ya Akershus (Akershus festning) Tunamsubiri kwa hamu!!

No comments: