Unafikiria kutoa hela zako benki
na kuziweka kwenye godoro
kabla ya mwaka mpya?
Fikiria tena!
Je, unafikiria kutoa hela zako benki zote na kuziweka kwenye godoro mpaka mwaka mpya uanze na uzirudishe kwenye akaunti yako? Fikiria tena!
Mara nyingi watu hususan mamilionea na mabilionea, hutoa hela zao kwenye akaunti kabla ya mwaka mpya na kuzirudisha tena mwaka mpya unapoanza ili kukwepa kukwepa kulipa kodi ya mali (formue skatt/property tax) ya mwisho wa mwaka. Lakini jamaa wa idara ya kodi (skatteetaten) mwaka huu wamekuwa makini sana na hilo.
Mama mmoja mstahafu amekiona cha mtema kuni!
Jamaa wa kodi wamegundua kuwa mstahafu huyo ndio mchezo wake. Huwa anazitoa hela zake kabla ya mwisho wa mwaka, halafu anazirudisha mwaka mpya ukianza. Amegundulika kukwepa kulipa kodi ya karibu kroner milioni 24,5 (T.shs. 5,552,085,504.00) kwa kipindi alichokuwa anafanya mchezo huo wa kukwepa kulipa kodi. Kwa hela alizonazo, alitakiwa kulipa kroner 16.000,- (T.shs. 362,585.00 kila mwisho wa mwaka).
Mama huyo amepigwa faini ya Kroner 500 000,- (laki tano) au T.shs. 113,307,864.00. Hayo yamesemwa na mkurugunzi mkuu wa idara ya kodi, mashariki ya Norway, Bw. Jan-Egil Kristiansen.
Kristiansen ameshangazwa na wingi wa kesi za Wanorwejiani waliokamatwa kwa njia za kukwepa kulipa kodi za kumiliki mali. Mwaka jana kulikuwa na kesi 44 na mwaka huu kumekuwa na kesi 50.
Kesi kubwa mwaka huu ni ya mama mmoja aliyetoa Kroner milioni 6 na nusu kutoka kwenye akaunti yake akidhani jamaa wa kodi wamelala. Upelelezi wa kesi yake unaendelea.
1 comment:
Watanzania mmeona? Hatuko pekee yaetu.
Karibuni duniani kote...binadamu wanatafuta upenyo wa kukwepa kulipahela kwenye dola...
Post a Comment