Thursday, December 03, 2009

Unasafiri kwenda Denmark?




Kama una mpango wa kusafiri kwenda Denmark, basi hakikisha unachukua pasipoti yako, hata kama una uraia wa Norway. Kuanzia sasa serikali ya Denmark itaanza kuangalia pasipoti kwa wote watakaoingia nchini humo. Hii ni moja ya njia ya kuhakikisha ulinzi, kwenye matayarisho ya mkutano mkuu wa mazingira duniani utakaoanza Copenhagen wiki ijayo. Yeyote atayajaribu kuingia bila pasipoti atarudishwa anakotoka au anaweza hata kuwekwa kizuizini.


No comments: