Thursday, December 24, 2009

Volvo yanunuliwa na Wachina



Kwa wale wanaolalamika kuwa Wachina wanachukua Afrika kimachomacho, angalieni. Sasa wananunua Ulaya taratibu!!!



Volvo XC 90 PUV





Kampuni ya magari ya Kichina ya Zhenjian Geely Holding Group imenunua kampuni ya magari madogo ya Volvo. Msemaji wa Volvo amesema kuwa mauzo rasmi hayajafanyika, lakini makubaliano ya kwanza ya mauzo ya Volvo yameshafikiwa. Volvo inamilikiwa na Ford Motor ya Marekani. Hii ni kampuni kubwa ya pili ya Waswidi iliyokuwa hatari kwenda mrama. SAAB tayari inakaribia kuzama, kwa ni General Motor (GM), iliyokuwa ikimiliki SAAB imefikia uamuzi wa kuiacha SAAB ifilisike. Kuna matumaini finyu sana kuwa labda SAAB itaokolewa na kampuni moja ya magari ya Kiholanzi. Kampuni hiyo imetoa masharti kadhaa, kabla ya kutangaza rasmi kuwa inainunua SAAB.


Bofya hapa na soma kuhusu Geely toka Wikipedia


Bofya hapa na soma zaidi kuhusu Volvo toka Wikipedia

2 comments:

Anonymous said...

LAKINI WENZETU WANA UTARATIBU MZURI HATA KAMA WACHINA WAMENUNUA LAKINI BADO ITAITWA VOLVO, LAKINI KWA TANZANIA WANGEBADILI HATA JINA ,TUNGALI BADO VIONGOZI WETU MASILAHI MBELE KULIKO TAIFA

Mtambalike said...

Umenena!