Mke wa waziri akamatwa kwa
tuhuma za midaharati
Sheryl Cwele, ambaye ni mke wa waziri Siyabonga Cwele, amefikishwa mbele ya sheria, kujibu mashtaka ya kuhusika katika jaribio la kuingiza madawa ya kulevya aina ya Cocaine, nchini Afrika Kusini kutokea Brazil.
Inadaiwa kuwa Bi Cwele alimtumia mwanamke mmoja kusafirisha dawa hizo kutoka nchini Uturuki hadi Brazil, ambako alimchukua mwanamke mwingine na Bwana mmoja aliyefahamika kwa jina la Frank Nabolis, raia wa Nigeria, waliozisafirisha dawa hizo kutokea nchini Brazil na kujaribu kuziingiza nchini Afrika kusini, kabla ya kukamatwa na maafisa wa usalama. Sherly amekuwa akitumia wanawake wa Kizungu wa Afrika Kusini kwenye biashara yake hiyo ya madawa ya kulevya, ili wasishukiwe na vyombo vya usalama.
Mshtakiwa amewekwa rumande mpaka kesi yake itakaposikilizwa tena wiki ijayo.
More:

No comments:
Post a Comment