Sunday, January 31, 2010

Luanda, Angola

Misri mabingwa wa Afrika


Misri (The Pharaohs) imekuwa mabingwa wa Afrika
kwa mara ya tatu mfululizo, baada ya kuwafunga Ghana 1 – 0
Goli hilo lilifungwa na dakika ya 85 na Mohammed Nagi ”Gedo”.
Gedo ameweka historia ya soka kwa kuwa rizevu
aliyefunga kila mechi aliyocheza kwenye mashindano
na pia ni mfungaji wa magoli mengi kwenye
mashindano haya kwa magoli 5.
Misri inaongoza kwa kuchukua kombe la 
mataifa ya Afrika. Imekuwa mabingwa mwaka
1957, 1959, 1986, 1998, 2006, 2008 na 2010.

No comments: