Tuesday, February 02, 2010

Akamatwa akivusha kroner 
milioni mbili

Jamaa mmoja mwenye asili ya Lebanon amekamatwa mpakani Svinesund kati ya  Norway na Sweden, jana Jumatatu akijaribu kuvusha Kroner za Kinorweji milioni mbili chini ya kiti cha dereva (kama T.shs. 459,850,766). Yamesemwa na Bi. Wenche Fredriksen wa Idara ya Ushuru wa Forodha, kanda ya Mashariki.

Jamaa wa ushuru wa forodha walipomhoji, akadai kuwa aliahidiwa kupewa kroner 15.000,- na watu waliomtuma kuja Oslo kutoka Stockholm kuchukua furushi hilo la hela.

Polisi bado wamedai kuwa mpaka sasa hawajui kuwa kama hela hizo zinatokana na biashara haramu au vipi.

Hairuhusiwi kuchukua zaidi ya Kroner 25.000,- kuzitoa nje ya Norway bila ya kibali cha Benki kuu ya Norway (Norges Bank)

No comments: