Tuesday, February 23, 2010




Barua ya Papii Nguza
kwa Rais Kikwete



Barua hii ametumiwa Judith Wambura (Jide) LadyJayDee na ameruhusu itumike katika vyombo vya habari na mawasiliano ila shukrani na taratibu za kunakili zizingatiwe. Tafadhali zingatia hilo.


MF/NA: 836'04 Johnson Nguza (Papii Kocha)
Gereza Kuu Ukonga
S.L.P 9091
Dar es Salaam


Mh. Rais Jamhuri ya Muungano Tanzania


YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.

Husika na somo hilo hapo juu. Mimi ni mfungwa katika gereza kuu Ukonga.


Kwa heshma na taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya ki MUNGU ulionayo dhidi ya binadamu wenzako pamoja na mamlaka uliokabidhiwa na jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Naanguka na kushika miguu yako mitukufu muheshimiwa rais.
Na kuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa rais
Kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani, niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu.

Mh.Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo. Mpaka sasa natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako mitukufu Mh. Rais.

Naomba huruma yako muheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninaehitaji huruma yako wewe mzazi.

Natumaini kauli yako ya mwisho ndio itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu

Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu.
Mungu akubariki


Wako mtiifu
NO:836'04
JOHNSON NGUZA (PAPII KOCHA)

Na huo ndio mwisho wa barua alionitumia Papii ili imfikie Mh. Rais


No comments: