Jinsi ya kutengeneza nywila
(Password) madhubuti
Na Da´ Subi
Jinsi ya kutengeneza nywila imara na madhubuti na jinsi ya kuepuka kutengeneza nywila nyepesi, legevu, nyong'onyevu, jinga kabisa na ambazo ni rahisi kubambwa.
Tarakimu au herufi zinazofuatana (similar or sequencials).
Mfano: "12345678," "88888888," "abcdefg," au herufi zinazofuatana juuna chini ya kibodi kama vile yhbujnikm ama xswcdevfr
Usitumie alama ambazo ni rahisi kufahamika kuwa zimetumika badala ya herufi. Mfano: '1' badala ya 'i' au '@' badala ya 'a' au '0' badala ya 'O' au 'E' badala ya '3' au "P@ssw0rd" nk.
Usitumie jina lako la login au username wala sehemu ya majina yako rasmi au tarehe ya kuzaliwa au namba ya TIN au SSN au sanduku la posta au namba ya simu au namba ya nyumba unamoishi nk kutengenezea nywila.
Unaweza kushangaa, 'wezi wanawezaje kupata taarifa hizi zote?', ni rahisi. Wezi hutafuta habari zako kwa kina kupitia vielelezo vyako kwenye mitandao jamii kama vile Facebook, Twitter, Hi5, LinkedIn, nk. vile vile katika Wasifu wako wa CV au Resume, na kwenye tovuti yoyote ile ambamo umeacha taarifa zako na ikawa rahisi kuzipata kwa njia mitandao ya utafutaji (search engines) kama vile google, yahoo, ask nk.
Usitumie meneno ya kwenye kamusi ya lugha yoyote.
Utawakuta baadhi ya watu hutengeneza nyila kwa kutumia maneno ya kamusi na kuyageuza kinyumenyume au kuandika maneno ya kutusi nk. Hii ni rahisi kwa wezi kutumia software ya word-scramble na kupata aina mbalimbali ya maneno yanayoweza kutengenezwa kutoka katika neno hilo, hasa pale wanapokuwa wameshapata hint'. Kumbuka kuwa wapo watu wanaolipwa kwa kufanya kazi ya kuiba nywila, hivyo ni ajira na huwza kuifanya kazi hii kwa saa hata kumi mfululizo ikiwa wameahidiwa donge nono na hasa kama walishawahi kufanikiwa kung'amua nywila nyingine.
Acha tabia ya kutumia nywila moja kwa akaunti zako zote. Do NOT use only one password for all your accounts
Wapo baadhi ya watu ambao hupenda kujifanyia urahisi kwa kutumia nywila moja kwa ajili ya akaunti zao mbalimbali, kwa mfano, mtu anatumia nywila ya Facebook kufungulia Twitter au LinkedIn. Hii ni makosa kabisa. Ukitumia nywila moja kwa akaunti zako zote, siku mwizi atakapofanikiwa kuibamba moja, basi utakuwa umewarahisihia kazi ya kujaribu akaunti zako zote kukamilisha ujangili wao.
Kuwa mwangalifu unapotengeneza neno la siri la kukumbushia anwani yako pale utakapoipoteza. (Be careful with password recovery questions)
Mara nyingi unaposahau anwani yako, huwa unatakiwa kubofya neno, 'I forgot my password' na hapo huanza utaratibu wa kukuuliza neno la siri kabla ya kukurekebishia nywila yako. Kuwa mwangalifu na swali la siri pamoja na jibu lake. Mara nyingi kampuni au huduma husika watakupa maswali yaliyoandaliwa ambapo utatakiwa kuchagua mojawapo na kulitolea jibu. Kwa bahati mbaya au nzuri, maswali haya ni rahisi kwa mtu kuyakisia. Mfano, Shule yako ya msingi inaitwaje? Swali kama hili ni rahisi kwa mtu anayekufahamu kulijua hasa kama mlisoma pamoja shule ya msingi au ni jirani yako au alisoma nawe shule ya Sekondari au Chuo au anafanya kazi nawe au ndugu, jamaa na rafiki mnayefahamiana akawahi kutamka kuwa mmesoma pamoja, huyu anaweza kupata urahisi wa kuiba nywila yako.
Jiepushe na matumizi ya stoo za mtandaoni (online storage)
Mwizi atakapoweza kuiba online storage yako, ni rahisi sana kuiba nywila na taarifa zako ikiwa umezihifadhi humo.
Mwizi atakapoweza kuiba online storage yako, ni rahisi sana kuiba nywila na taarifa zako ikiwa umezihifadhi humo.
Ukitaka kusoma vidokezo vya namna ya matumizi mazuri na angalifu ya emails, tafadhali peruzi kwenye lebo katika 'Computer Or Email Tips & Tricks'. (To read previous email tips, use the search box located above the page or click through 'Computer Or Email Tips & Tricks' under the labels).

No comments:
Post a Comment