Kroner milioni 40 zaibiwa
Kwenye duka la vito vya thamani.
Duka la Gullborgen, Storgata Oslo.
Dula la vito vya thamani la Gullborgen lililoko Storgata, mjini Oslo, limeibiwa kroner milioni 40 wikiendi ya juzi. Yamesemwa na msemaji wa polisi Oslo, John Roger Lund.
Wiki huu ni wa pili wa aina yake kwa wezi kuondoka na hela au vito vya thamani vyenye gharama hizo kubwa kiasi hicho*. Dhahabu yote, almasi zote na hela zilizokuwa kwenye masanduku maalumu ya kuhifahi vito vya thamani na hela yaliyokuwa lelo (basement).
Wezi hao walichukua kila kitu mpaka na kamera za ulinzi kwenye duka hilo.
· Wizi wa kwanza ni wa NOKAS uliotokea Stavanger 4 Aprili 2004 ambazo majambazi yaliiba kroner zinazosadikiwa kuwa zaidi ya milioni 60. Zaidi kuhusu NOKAS bofya na soma.

No comments:
Post a Comment