Kwa presha hizi, itakuwa viharusi badala ya harusi
Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,
Uzitoni Street,
Bongo.
Uzitoni Street,
Bongo.
Mpenzi Frank,
Waniuaua kipenzi waniuaua
Waniuaua kipenzi waniuaua
Nakuwazia kila saa waniuaua
Bila wewe sina raha waniuaua
Waniuaua kipenzi waniuaua
Nakuwazia kila saa waniuaua
Bila wewe sina raha waniuaua
Unasikia mpenzi? Na unasikia sauti yangu nyororo ikiimba huku macho yanakurembulia. Wacha wewe! Amini usiamini nakupenda sana. Sijui na hali yako ikoje wiki hii lakini mimi nimelegea kwa kukuwazia tu. Jitunze mpenzi wangu nikutuze.
Lakini mwaka huu sijui itakuwaje. Kama presha iko hivi mapema namna hii, kufika katikati ya mwaka itakuwaje. Itakuwa viharusi badala ya harusi. Nakuambia!

No comments:
Post a Comment