Saturday, February 06, 2010

Oslo, Norway

Madereva wa taxi wafanya mgomo kuamkia leo.



Saa 8 hadi saa 10 za usiku wa manane kuamkia leo madereva wa taxi Waislamu hapa Oslo walifanya mgomo wa kupinga kuchapishwa vikatuni vinavyomwonyesha Mtume Muhammad (S.A.W) kama nguruwe kwenye gazeti la Dagbladet . Jumatano wiki hii, gazeti la Dagbladet lilichapishwa vikatuni hivyo kwenye ukurasa wambele, kufuatilia kwa vikatuni hivyo kuonekana kwenye ukurasa wa Facebook wa idara ya usalama wa taifa ya Norway, Politiets sikkerhetstjeneste (PST). PST tayari wameshaviondoa vikatuni hivyo na kuomba msamaha kuwa walishindwa kuviondoa haraka baada ya mtu mmoja kuviweka kwenye ukurasa wao wa Facebook.

No comments: