Madereva wa taxi wagoma tena leo asubuhi!
Madereva wa taxi Waislamu hapa Oslo leo asubuhi waligoma kuendesha kwa masaa matatu kupinga kitendo cha gazeti la Dagbladet kuchapisha kikatuni cha Mtume Muhammad (S.A.W) akionekana kama nguruwe. Kikatuni hicho kilichapishwa kwenye Dagbladet Jumatano wiki iliyopita.
Dagbladet walichapisha kikatuni hicho kufuatilia kuonekana kwa kikatuni hicho kwenye ukurasa wa Facebook wa idara ya usalama wa taifa ya Norway, Politiets sikkerhetstjeneste (PST). PST tayari wameshaviondoa kikatuni hicho na kuomba msamaha kuwa walishindwa kukiondoa haraka baada ya mtu mmoja kuviweka kwenye ukurasa wao wa Facebook.
Mgomo wa kwanza wa madereva hao wa taxi ulifanywa usiku wa kuamkia Jumamosi wikiendi iliyopita.

No comments:
Post a Comment