Atia mafuta ya taa kwenye moto!
Mohyeldeen Mohammad akiwa kwenye maandamano wiki moja iliyopita
Baada ya maandamano wiki moja iliyopita ya Waislamu kama 3000 hivi waliokuwa wakipinga gazeti la Dagbladet kuchapisha kikatuni cha Mtume Muhammad (S.A.W) akionekana kama nguruwe, kijana Mohyeldeen Mohammad (24) kutoka Larvik hapa Norway, amezua mjadala hapa Norway kiasi ambacho idara ya usalama wa taifa ya Norway (Politiets sikkerhetstjeneste, PST) imeingiwa na wasiwasi.
Mohyeldeen alikuwa mmoja wa wasemaji kwenye maandamano hayo (bofya kwa hadidu rejea). Alisema kuwa
”Norway iache kuwadhalilisha Waislamu, vinginevyo kutatokea kama kilichotokea Septemba 11”
Msemo huu ndio umeacha kumbukumbu pekee baada ya maandamano hayo.
Licha ya kuwa maandamano hayo yalikuwa ya amani bila fujo za aina yoyote, msemo huo umelikasirisha taifa zima la Norway, wakiwemo Waislamu wote wenye itikadi za kati zenye upendo wa amani.
Mohyeldeen anayesomea theolojia ya sharia kwenye Chuo Kikuu Cha Kiislam cha Madina (Islamic University of Madinah, Saudi Arabia), ameongeza mafuta ya taa kwenye moto aliouwasha pale alipowatishia waandishi wawili wa habari wa Dagbladet kuwa atawaua/watauawa na aliposema kuwa:
”Watu wa jinsia moja wanaopendana wapigwe mawe hadi kufa”
Jana idara ya Usalama wa taifa ya Norway, PST kwenye mkutano wake wa kila mwaka kutoa tathmini ya hali ya usalama wa nchi, imeonyesha wasiwasi wake jinsi baadhi ya vijana wa Kiislam waliozaliwa na kukulia hapa Norway wanavyojiingiza kwenye itikadi kali za kidini kwa kusaidiwa na baadhi ya vikundi vya kidini. PST imesema kuwa vijana wake wa kazi wanafuatilia kwa karibu sana nyendo za vijana na waislamu wote wenye itikadi kali za kidini.
Na mhariri wa blogu.

1 comment:
Norway ni inchi ya kikristo na wanasheria zao na utamaduni wao. Kama wewe u mwislam na unataka uislam basi Hama nenda kaishi uarabuni kwenye dini ya kiislam. Usiwabadilishie wanowejieni utamaduni na dini yao.
Baniani mbaya kiatu chake dawa?
Wazungu wakienda uarabuni wanaishi Kama waarabu na sisi tuishio uzunguni tuishi Kama wao.
Dunia mzima watu Wa jinsia moja wanafanya mapenzi hata Huko uarabuni wasenge kibao na mabasha.
Post a Comment