Polisi na waandamanaji wapigana
Kuanzia jana jioni kumekuwa na mapigano kati ya polisi na waandamanaji wanaopinga watu waliokuwa wamevamia na kukaa bure kwenye jengo la Manispaa ya Oslo mtaa wa Hausmann namba 42, kufukuzwa kwenye jengo hilo.
Polisi walitumia mabomu ya machozi na maji ya kasi kuwatawanya waandamanaji hao, waandamanaji walijibu kwa kuwarushia polisi matofali , chupa na nondo. Machafuko hayo yaliendelea hadi kwenye usiku wa manane. Hali haijulikani itakuwaje leo hii.
Karibu waandamanaji 100 – 150 wamekamatwa na wameswekwa lupango.
No comments:
Post a Comment