Ruzuku kwa vyama vya wageni:
Dawa iko jikoni!
Katibu mkuu, Bi. Henriette Westhrin, wizara ya watoto, usawa na ujumlisho wa jamii,
kwenye gazeti la Aftenposten, Jumamosi 27.02.2010.
Wizara ya watoto, usawa na ujumlisho wa jamii (Barne-, likestillings-og inkluderingsdepartmentet, BDL) itafuatilia kwa makini na ukaribu utoaji hela na ruzuku kwa vyama vya wageni. Haya yamesemwa na katibu mkuu wa wizara hiyo, Bi. Henriette Westhrin (SV), baada ya suala la ruzuku kuandikwa sana wiki hii na gazeti la kila siku la hapa, Aftenposten (bofya hapa kwa hadidu rejea).
Wizara imesema kuwa idara yake inayoshughulikia ruzuku kwa vyama vya wageni, IMDi (Directorate of Integration and Divesity) imepewa jukumu la kufuatilia hili suala la ruzuku kwa kufuata kwa makini maelekezo ya wizara ya mwaka 2009.
Wadau na wote wanaopinga ruzuku kutolewa kwa vyama vya wageni, hususani vyama vya upinzani, havijaridhishwa na majibu mepesi ya suala hili yaliyotolewa na katibu mkuu. Wamesema kuwa hayo ya kufuatilia kwa makini na kwa karibu si ya jana, wameyasikia siku nyingi na mpaka leo mwendo ni ule ule kuwa vyama vyenye wajanja wanaojua “miundo” ndivyo vinavyopata ruzuku nyingi. Na hivi ndivyo vinavyojificha kwenye miamvuli ya “ugeni” badala ya kujumuika na wazawa kwenye shughuli zao.
Mhariri
No comments:
Post a Comment