Tuesday, March 30, 2010

Ashakum si matusi!!! *Warning* Must Be 18 years Or Older To View!!!

Eryikah Badu – Window Seat
Atembea mtaani uchi wa mnyama!


Mwanamziki Eryikah Badu amewashangaza wakazi wa Dallas kwenye kideo cha wimbo wake mpya uitwao ”Window Seat”. Kwenye kideo hicho, Eryikah anavua nguo sehemu Rais John F. Kennedy alipopigwa risasi na kuuawa 22 Novemba 1963. Sehemu ya mwisho ya kideo kinaonyesha Eryikah anaanguka sehemu JFK alipopigwa risasi. Wakati kideo kikichukuliwa, kulikuwa na watoto na wazazi wao, na wengi walishangazwa na kitendo cha chake cha kuvua nguo na kubaki uchi wa mnyama, tarehe 17 Machi 2010!

Mwanamama msemaji wa polisi wa Dallas, Koplo Janice Crowther amesema kuwa Eryikah hatashtakiwa, kwani mpaka sasa hakuna aliyelalamikia kitendo chake kwenye uchukuaji wa kideo hicho!

Eryikah Badu alizaliwa Dallas na ndiko anakoishi na watoto wake watatu; mmoja wa mwaka mmoja, miaka 5 na miaka 12.


No comments: