Wednesday, March 31, 2010

Nedre Romerike, Akershus

Abambwa na kokeini kwenye wigi:
Afungwa jela miaka miwili na nusu.
Mwanamke mmoja Mholanzi (45), amehukumiwa kifungo cha miaka miwili na nusu jela kwenye mahakama ya Nedre Romerike.

Mwanamke huyo alikamatwa 27. Desemba 2009 kwenye uwanja wa ndege wa Oslo Gardemoen, akitokea Düsseldorf, Ujerumani. Alikamatwa akiwa ameficha kokeini kilo moja kwenye wigi alillovaa.

Aliiambia mahakama hiyo kuwa alitumwa na Waafrika flani ambao hawajui kuingiza kokeini hiyo, na kuwa walimwahidi wangemlipa Euro 3000,- sawa na kroner 25000,-

No comments: