Wednesday, March 24, 2010

Njombe, Tanzania

Binti atoroka kutumikishwa bar
Njombe ahukumiwa na polisi


Binti yatima mwenye umri wa miaka 14 mkazi wa mji mwema Mafinga wilaya ya Mufindi Mariam Nyagawa (pichani ) amenusulika kubakwa usiku wa manane na kuishia kukamatwa na polisi mjini Njombe baada ya kukimbia katika eneo lake la kazi katika bar moja maarufu mjini Njombe inayofahamika kwa jina la Sovyo ambako alikuwa akitumikishwa kufanya kazi ya kuuza bar kwa ujira wa shilingi 10,000 kwa mwezi.

Binti huyo aliuleza mtandao huu wa http://francisgodwin.blogspot.com nje ya kituo cha polisi Njombe kuwa tukio hilo lilitokea jana machi 22 mwaka huu baada ya kufanya kazi katika bar hiyo kwa muda wa siku tatu bila kupumzika.

Anasema kuwa pamoja na kufanya kazi hiyo ya kuuza pombe bado alikuwa akipewa wanaume ambao sawa baba yake wa kwenda kulala nao hali iliyopelekea kuiona kazi hiyo chungu kwake na kuamua kutoroka usiku wa manane.

Hata hivyo alisema kabla ya kuja Njombe alirubuniwa na mwanamke mmoja kuwa kuna kazi nzuri ya kufanya ambayo ingemwezesha kupata fedha za haraka za kumwezesha kulipa karo ya shule ya ufundi ili kuendelea na mafunzo ya kushona baada ya kufeli mtihani wa Taifa wa darasa la saba mwaka jana.

Ila baada ya kufika Njombe anadai ilipewa nguo fupi na kupelekwa katika bar hiyo kwa ajili ya kufanya kazi ya ukahaba ambayo haiwezi .

Kutokana na polisi wa doria kumkamata usiku wa manane akiwa mbioni kurudi Mafinga kwa kutembea kwa miguu walimpeleka kituo cha polisi ambako alilazwa hadi asubuhi na kutokana na kujieleza waliweza kumwachia katika kesi ya uzembe na uzurulaji kwa kumpa hukumu ya kudeki choo kwa mikono pamoja na nyumba mbili za askari polisi.

Hata hivyo kutokana na hali hiyo ya binti huyo kutojua wapi kwa kwenda mmiliki wa mtandao huu aliweza kuwasiliana na mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu pamoja na kumpa nauli ya shilingi 10,000 kwa ajili ya kurudi Mafinga ili uongozi wa wilaya kuweza kumsaidia kuendesha maisha yake hata kumtafutia shule ya kusoma japo jitihada za mtandao huu kumsomesha zinaendelea kufanywa.

Pamoja na mkasa wa binti huyo bado uchunguzi wa kina uliofanywa na mtandao huu katika bae nyingi za mji wa Njombe idadi kubwa ya wahudumu wake ni watoto wa miaka 12,14 na 20 jambo ambalo linapaswa uongozi wa wilaya kufanya msako ili kuwarejesha shule watoto hao.

No comments: