Wednesday, March 24, 2010

Bergen, Norway


Aiachaji iPhone usiku kuamka
chaja imeungua!


Sanel Sarajlija akionyesha jinsi iPhone yake ilivyoungua.
Picha na Emil Ahlén na Hallgeir Vågenes.



Sanel Sarajlija (23) aliweka iPhone yake kwenye chaja akaenda kulala, alipoamka akapatwa na mshtuko wa mwaka, kwani chaja ilikuwa imeungua kwa umeme. Tukio hili limetokea Bergen, kuamkia leo.


Hili si tukio la kwanza kwa chaja za iPhone kuungua kwa umeme. Mwaka 2008 tukio kama hili lilimtokea Emil Ahlén nchini Sweden.

Gazeti la VG, limejaribu bila mafanikio kuwatafuta Apple juu ya hili tukio. Petter Arhrnstedt, msemaji wa Apple Norway amekubali wataalamu wa Apple kuichukua simu ya Sanel wakaifanyie uchunguzi, lakini amekataa kusema lolote juu ya tukio hili, wala lilie lililotokea Sweden mwaka 2008, ambalo mpaka leo wamekataa kulijibu.

Wataalamu wa TEKNOHAMA wanaonya watumiaji wa iPhone kuitumia program moja inayoitwa ”Sleep Cycle” ambayo unatakiwa uiweke iPhone kwenye mto, wakati umelala huku ikiwa inaangalia jinsi usingizi wako ulivyo.

Sleep Cycle imetengenezwa na  Lexware Labs ya Gothenburg, Sweden. Wataalamu wa mambo ya moto wanaonya kuchaji simu yoyote ya mkononi usiku huku ukiwa umelala, wanasema ni bora kuchaji huku mwenyewe ukiwa macho. Kuna matukio mengi ya simu za mkononi kuungua usiku huku zikichajiwa.

No comments: