Kaimu Rais Goodluck Jonathan
Avunja baraza la mawaziri.
Rais Jonathan amelivunja baraza la mawaziri ghafla, bila kutoa taarifa kwa mawaziri wake, amesema Bi. Dora Akunyili, aliyekuwa waziri wa habari.
Hivi karibuni Rais Jonathan, alimshusha wadhifa waziri wa sheria na kumfukuza kazi , mshauri mkuu wa masuala ya usalama wa taifa. Wote hao walikuwa maswahiba wa Shehu Yar´Adua; Rais ambaye ni mgonjwa kwa muda mrefu sasa.
Kutokana na katiba ya Naijeria, magavana wa majimbo 36 na viongozi wa vyama vinavyounda serikali, ndivyo vitakavyopendekeza majina ya mawaziri wapya, halafu wapitishwe na seneti ya Naijeria, kitu ambacho kitachukua muda mrefu.

No comments:
Post a Comment