Tuesday, March 02, 2010

Katika historia

Majira ya Chipuo (Spring)



Maua ya kwanza yanayoanza kuchipua kwenye Majira ya Chipuo. haya yanaonekana yakichipua huku kukiwa na barafu.


Leo kwa mara ya kwanza hapa Oslo (Mashariki ya Norway) jua limetoka kutwa nzima. Kulikuwa na halijoto. Hizi ni dalili za majira ya Chipuo (Spring).

Kama tunavyojua mwezi Machi ni wa tatu kwenye kalenda ya Gregorian; kalenda tunayotumia ya Januari hadi Desemba. Ni mmoja kati ya miezi saba ya mwaka yenye siku thelathini na moja.

Jina la Machi linatoka kwenye historia ya Ugiriki ya kale. Kwenye enzi za Roma, Machi ulikuwa mwezi wa kwanza wa mwaka na umepewa jina hilo kutoka kwa Martius, Mungu wa enzi za Roma wa vita. Mwaka kwenye enzi za utawala wa Roma, ulikuwa na miezi kumi.

Kihistoria, mwezi wa Machi ni mwezi wa mwanzo wa majira ya Chipuo (Spring) kwenye mabara yenye misimu minne kwa mwaka, yaani Majira ya Kiangazi/joto (Summer), majira ya Kupukutika (Autumn), Majira ya theluji/Kipupwe (Winter) na Majira ya Chipuo (Spring).

Miezi ya majira ya Chipuo huku nchi za Nordic (Norway, Sweden, Denmark, Finland, Iceland na visiwa vya Faeroe) ni Machi, Aprili na Mei.

Hivyo basi, tunatarajia kuwa Majira ya Chipuo ndiyo yameanza. Si ajabu hapa Norway, theluji kuanguka hadi mwezi wa nne.

Tukio kubwa la kukumbukwa mwezi Machi mwaka huu ni siku ya wanawake duniani, itakayoadhimishwa Jumatatu, tarehe 8 Machi.

2 comments:

Anonymous said...

NILIKUWA SIJUI KUWA SPRING KWA KISWAHILI NI MAJIRA YA CHIPUO.

ASANTENI SANA!

Anonymous said...

Naomba kuuliza hivi Tanzania tuna hayo majira ya vipindi vinne vya mwaka?

Kama tunavyo tafadhari naomba unisaidie kuwa summer ni mwezi wa ngapi hadi wangapi hadi vipindi vyote.

Kila mara niulizwapo swali hili huwa sijiamini kujibu na vile vile kwa manufaa ya wengine pia.


Natanguliza shukrani.