Miaka 30 amekuwa akiishi
porini hata kwenye
majira ya theluji
Huyu jamaa Mnorwejiani, Sverre Nøkling kwa miaka 30 amekuwa kiishi porini na hata kwenye majira ya theluji amekuwa akijichimbia makazi yake kwenye theluji. Anasema kuwa hata matatizo ya kuishi na binadamu wengine, ile yeye mwenyewe ameamua kuishi kama anavyoishi. Sverre ana karibu miaka 60 sasa, anasema siku inaanza kwa kumka na kutembea masafa marefu halafu na kurudi anakokaa.
Anaishi kama binadamu walivyokuwa wanaishi binadamu miaka elfu iliyopita kwa mahitaji yake ya kila siku, kama chakula na mengineyo. Tofauti ni kuwa ana nyenzo za kisasa za kumsaidia kama nguo, kujipasha moto, na kuchemsha maji n.k.
Juzi Ijumaa 12.3.2010 sinema ya maisha ya Sverre ilizinduliwa.




No comments:
Post a Comment